SEA Vision Ltd ni Kampuni iliyotengenezwa kutokana na maono ya mbali (vision) ya muasisi wake ndugu Shabani Sululu.

Neno “SEA” limetokana na herufi za mwanzo za majina ya watu waliohusika kwenye mchakato wa awali wa uundwaji wa Kampuni.
Baada ya kuwa na wazo la kumiliki Kampuni kwa kushirikiana na wanafunzi wenzake ambao wengi walikuwa ni kutoka Kenya ambao walikutana chuo kikuu cha Makerere pale Uganda, mtendaji mkuu wa Kampuni ndugu Shabani Sululu aliamua kuwashirikisha wazo hilo rafiki zake wawili wa kitanzania
Wakiwa chuo kikuu cha Makerere, Shabani Sululu na wenzake waliandaa mpango wa kuanzisha biashara (business plan) na kupeana malengo kwamba baada ya kumaliza shahada yao ya kwanza ya biashara ya kimataifa (degree in International business) kila mmoja wao arudi nchini kwake na aanze utekelezaji.Baadae waungane kwa pamoja na kuunda Kampuni kubwa ambayo itafanya kazi kwenye nchi za  Afrika Mashariki na baadae nje ya mipaka ya Afrika Mashariki.
Baada ya kumaliza masomo alirejea Tanzania na kuanza kutafuta kazi ikiwa ni sehemu ya kutengeneza mtaji wa kifedha ambao ulifanikiwa kupata ajira kwenye benki ya Stanbic kama “bank Teller” mnamo tarehe 20.12.2012 ikiwa ni miezi sits tangu arejee nchini.
Akiwa Stanbic Shabani alitengeneza ukaribu na watu wengi wa rika mbalimbali ndani na nje ya benki na kila alipopata nafasi aliitumia kuwashirikisha wazi alilokuwanalo la kuunda Kampuni.
Alitamani apate vijana wenzake kwenye uwezo na elimu tofauti tofauti kama uhasibu, masuala ya teknolojia, biashara, sheria na kadhalika. Lengo hasa lilikuwa ni kuhakikisha hawapati changamoto za kuwalipa watu wenye utaalamu kwenye nyanja hizo na badala yake kila mmoja wao atumie elimu na na kipawa chake kuhakikisha Kampuni inasonga mbele. Awali alielekea kufanikiwa kwa kupata vinana takribani kumi na tano (15).
Wakaunda kundi la kuwasiliana kwa simu (watsup) na mikutano karibu yote ikawa inafanyika bila kulazimisha kukutana. Makutano ya wote yalikuwa ni kwaajili ya masuala nyeti sana.

Wakaanza kuchangishana fedha kila mwezi. Baada ya miezi minne kukatokea mfaralano ambao kimsingi ulihusisha wadau wakubwa watatu waliohusika kuanzia hatua za awali za uundwaji wa Kampuni. Mgogoro huo ukapelekea wadau karibu wote kujitoa kwenye kundi na ndipo Shabani alipomtafuta kijana mwingine ambae aliamini angeweza kuendana na falsafa na malengo mapana ya baadae na kuamua kuzungumza na ndugu Ipyana Mwakanosya. Baada ya mazungumzo walikubaliana kuendelea na wazo la kuunda kampuni na wakafanya marekebisho kidogo ya jina la kampuni kutoka lile la awali LA “SEA Vision 2018 LTD” na kuwa “SEA Vision LTD” ili historia isifutike moja kwa moja na safari ikaanzia hapo.